Covid-19:Watu 18 waaga dunia,433 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 395 wamepona corona,18 waaga dunia
  • Kufikia leoo kenya imesajili idadi jumla ya 173,072 visa vya maambukizi ya cocona, kutoka kwa jumla sampuli ya 1,840,889

Kenya imerekodi visa 433 vipya vya maambukizi ya corona, kutoka kwa sampuli 4,479 zilizopimwa chini ya saa 24.

Kati ya visa hivyo 415 ni wakenya huku 18 wakiwa raia wa kigeni, pia 247 ni wanaume huku 186 wakiwa ni wagonjwa wa kike.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 98.

Kufikia leoo kenya imesajili idadi jumla ya 173,072 visa vya maambukizi ya cocona, kutoka kwa jumla sampuli ya 1,840,889

Kulingana na twakimu za wizara ya afya watu 395 wamepona corona na kufikisha idadi jumla ya 118,621 ya watu waliopona corona.

Watu 262 wamepona huku wakipokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 133 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kuna wagonjwa 1,125 waliolazwa hospitalini huku wagonjwa 4,895 wakipokea matibabu wakiwa nyumbani.

Watu 18 wamepona virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 3,326 watu walioaga dunia.

Vile vile kuna wagonjwa 111 ambao wamelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi ICU.

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya kwanza imefika 978,127  huku idadi ya waliopokea chanjo ya pili ikifika 27,382.