KILIO CHA HAKI

Baba atuhumiwa kunajisi mabinti wake wawili wa miaka 4 na 6

Rutto, 49, anadaiwa kuwanajisi mabinti wake wawili baada ya kutengana na mkewe

Muhtasari

•Mwalimu wa msichana yule wa miaka 6 aligundua kuwa mwanafunzi wake hakuwa anaweza kutembea vizuri na aliskuwa analia mara kwa mara

•Mazungumzo na dada hao wawili yalifichua kuwa  wamekuwa wakiishi na baba yao tangu kuondoka kwa mama yao.

crime scene 1
crime scene 1

Polisi upande wa Iten wanazuilia mwanaume mmoja anayetuhumiwa kunajisi wanawe wawili wa miaka 4 na 6.

Luka Rutto, 49, anadaiwa kuwanajisi mabinti wake wawili wakati akiishi nao baada ya  kutengana na mke wake.

Imeripotiwa kuwa mwalimu wa msichana yule wa miaka 6 aligundua kuwa mwanafunzi wake hakuwa anaweza kutembea vizuri na aliskuwa analia mara kwa mara. Jambo ambalo lilimfanya mwalimu kutaka kujua kipi  kilichokuwa tatizo.

Juhudi za kupata majibu ziliangulia patupu kwani msichana huyo hakutaka kueleza ukweli kuhusiana na yaliyokuwa yamejiri.

Kimya chake kilimpelekea mwalimu huyo kumuita dadake wa miaka minne ambaye pia alishuhudia ugumu kutembea. 

Hapo mwalimu huyo akajulisha mwaalimu mkuu  wa shule hiyo kuhusiana na jambo hilo la kutatanisha.

Mazungumzo na dada hao wawili yalifichua kuwa  wamekuwa wakiishi na baba yao tangu kuondoka kwa mama yao.

Kufuatia hayo, mwalimu mkuu aliwaarifu maafisa wa polisi ili kuchukuliwa kwa hatua zaidi na baba yule akatiwa mbaroni jioni ya siku ya Jumatano huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

Vipimo vya kidaktari katika hospitali ya Iten vilithibitisha kuwa dada wale wawili kweli walikuwa wamenajisiwa. 

Mshukiwa huyo wa kitendo hicho  cha aibu ataendelea kuzuiliwa wakati upelelezi zaidi kuhusiana na kitendo hicho unaendelea.