Covid-19:Viwango vya maambukizi ya corona vimefika asilimia 8.0 huku 341 wakipona virusi hivyo

Muhtasari
  • Katika visa hivi vipya, 174 ni raia wa Kenya huku 14 akiwa raia wa kigeni,102 ni wa kiume na  ni 86 wanawake
  • Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 85
  • Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 8.0%
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya imerekodi visa 188 vipya vya maambukizi  ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 2,354 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 188,942 kutoka kwa sampuli 2,018,013.

Katika visa hivi vipya, 174 ni raia wa Kenya huku 14 akiwa raia wa kigeni,102 ni wa kiume na  ni 86 wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 85.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 8.0%.

Watu 341 wamepona virusi vya corona,250 walipona wakiwa nyumbani huku 91 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 179,861 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba Mtu 1 ameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,723  watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,062 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,381 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 120  wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).