Makali ya corona: Watu 16 waaga dunia huku 945 wakipatikana na corona

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa vipya 945 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,295  chini ya saa 24 zilizopita
  • Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 201,954 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 13.0%
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 910 ni wakenya ilhali 35 ni raia wa kigeni,481 ni wanaume huku 364 wakiwa wanawake
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya imesajili visa vipya 945 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,295  chini ya saa 24 zilizopita.

Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 201,954 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 13.0%.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 910 ni wakenya ilhali 35 ni raia wa kigeni,481 ni wanaume huku 364 wakiwa wanawake.

Kulingana na wizara ya afya watu 16 wameaga dunia kutokana na viruis vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 3,926 ya walioaga dunia.

Jumla ya wagonjwa 216 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni  188,438, 252 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 64 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa  1,432  ambao wamelazwa hospitalini,3,975 wamejitenga nyumbani.

Pia kuna wagonjwa 175 kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 1,712,550.