Makali ya corona: Watu 700 wapona,444 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 430 ni wakenya ilhali 14 ni raia wa kigeni,242 ni wanaume huku 202 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 245,781 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 5.9%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Kenya imesajili visa 444 vipya vya  maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 7,511 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 430 ni wakenya ilhali 14 ni raia wa kigeni,242 ni wanaume huku 202 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 245,781 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 5.9%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,486,331.

Mgonjwa wa umri wa chini ana wiki tatu ilhali mwenye umri wa juu ana miaka 90

Hata hivyo watu 4 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,965 ya walioaga dunia.

Aidha watu 700 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 236,169, 321 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 379 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,472 ambao wamelazwa hospitalini, 3,309 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 119 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).