Covid-19:Watu 170 wapatikana na corona,213 wapona,3 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 251,483 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 3.7%
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,617,700
Waziri wa afya Mutahi Kagwe
Image: MoH

Watu 170 wamepatikana na  maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,648 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 166 ni wakenya ilhali 4 ni raia wa kigeni,82 ni wanaume huku 88 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 251,483 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 3.7%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,617,700.

Vile vile watu 213 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 244,746,111 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 102 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hata hivyo watu 3 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,198 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 661 ambao wamelazwa hospitalini, 1,668 wamejitenga nyumbani.

HUku hayo yakijiri kuna wagonjwa 37 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 4,273,664.