Moto wateketeza soko ya Gikomba kwa mara nyingine

Chanzo cha moto huo bado hakijatambulika.

Muhtasari

•Moto huo uliteketeza mali ya mamilioni ya pesa katika soko hiyo kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashiriki.

•Haya yanajiri masaa machache tu baada ya mahakama kuruhusu huduma ya mji wa Nairobi (NMS) kufurusha baadhi ya wauzaji wa Mitumba katika soko ile ili kupatia nafasi upanuaji wa zahanati ya  Pumwani Majengo.

Moto wateketeza soko ya Gikomba Novemba 8, 2021
Moto wateketeza soko ya Gikomba Novemba 8, 2021
Image: THE STAR// HANDOUT

Wapelelezi na wataalamu wa moto wametumwa katika soko la Gikomba kuchunguza kisa kingine cha moto uliotokea usiku wa kuamkia Jumatatu.

Moto huo uliteketeza mali ya mamilioni ya pesa katika soko hiyo kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashiriki.

Polisi wanasema takriban ekari tatu za ardhi ambazo zilikuwa na vibanda na nguo zimeteketezwa na moto huo uliozuka mwendo wa  saa sita usiku.

Wafanyibiashara wachache tu ndio waliweza kuokoa mali yao kwani moto ule ulienea kwa kasi mno ukiteketeza kila kitu kilichokuwa katika eneo lililoathirika.

Chanzo cha moto huo bado hakijatambulika.

Haya yanajiri masaa machache tu baada ya mahakama kuruhusu huduma ya mji wa Nairobi (NMS) kufurusha baadhi ya wauzaji wa Mitumba katika soko ile ili kupatia nafasi upanuaji wa zahanati ya  Pumwani Majengo.

Moto huo umekuja wakati ambapo serikali iliahidi kuweka kamera za CCTV hapo kushughulikia matukio hayo ya mara kwa mara. Tukio kama hilo lilitokea mahali hapo mwezi uliopita. Hakuna aliyekamatwa.