Makali ya corona:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,997,816

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo wote ni raia  wa kenya,6 ni wanaume huku 6 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,309  na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.7%
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,771,792
Waziri wa afya Mutahi Kagwe
Image: MoH

Kenya siku ya mesajili visa 12 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 1,730 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo wote ni raia  wa kenya,6 ni wanaume huku 6 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,309  na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.7%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,771,792.

Aidha watu 37 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,682,25 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 12 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Vile Vile watu 3 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,319

Kuna wagonjwa 381 ambao wamelazwa hospitalini, 1,027 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 24 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,997,816.