Covid-19:Watu 69 wapatikana na corona,80 wapona,3 waaga dunia

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo 66 ni wakenya huku 3 wakiwa raia wa kigeni,37 ni wanaume huku 32 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,453 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.3%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Kenya siku ya mesajili visa 69 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 5,354 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 66 ni wakenya huku 3 wakiwa raia wa kigeni,37 ni wanaume huku 32 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,453 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 1.3%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,780,991.

Aidha watu 80 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,791,44 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 36 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Vile Vile watu 3 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,325.

Kuna wagonjwa 362 ambao wamelazwa hospitalini, 1,013 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 23 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,168,086.