Makali ya corona:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,398,580

Muhtasari
  • Kuna wagonjwa 351 ambao wamelazwa hospitalini, 977 wamejitenga nyumbani
  • Vile vile kuna wagonjwa 20 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS

Kenya siku ya Jumatatu imesajili visa 18 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 3,982 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 13 ni wakenya huku 6 wakiwa raia wa kigeni,10 ni wanaume huku 8 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,728 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.5%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,801,983.

Aidha watu 21 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,975,16 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 5 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hii leo hamna mtu ambaye ameaga dunia kutokana na corona huku idadi jumla ya walioaga dunia ikifika 5,328.

Kuna wagonjwa 351 ambao wamelazwa hospitalini, 977 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 20 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 6,398,580.