SASA TV yake mhubiri James Ng'ang'a yapigwa marufuku kwa kupeperusha jumbe chafu hewani

SASA TV imeamurishwa kutekeleza maagizo hayo mara moja.

Muhtasari

•SASA TV pia imeagizwa kuhakikisha imepata  wafanyakazi wa kutosha na waliohitimu ambao wameidhinishwa ipasavyo na baraza la vyombo vya habari la Kenya (MCK) kabla ya kurejea hewani.

Pst James Ng'anga
Pst James Ng'anga
Image: HISANI

Shirika la mawasiliano ncini (CAK) limeagiza stesheni ya Sasa TV inayomilikiwa na kanisa la mhubiri James Ng'ang'a la Neno Evangelism Centre kusimamisha matangazo yake kwa kipindi cha miezi sita.

SASA TV pia imeagizwa kuhakikisha imepata  wafanyakazi wa kutosha na waliohitimu ambao wameidhinishwa ipasavyo na baraza la vyombo vya habari la Kenya (MCK) kabla ya kurejea hewani.

Hatua hii imefuatia uchunguzi uliotamatika ambao ulibaini stesheni hiyo ilipeperusha matangazo yasiyofaa katika kipindi cha familia yote kutazama mnamo Oktoba 3, 2021.

Uchunguzi ulibaini kwamba SASA TV kanuni za maadili ya uandishi wa Habari nchini Kenya kama ilivyoelekezwa kwenye katiba.

SASA TV imeamurisha kutekeleza maagizo hayo mara moja.

Mkurugenzi mkuu wa CAK, Ezra Chiloba ameagiza SASA TV kuhakikisha wafanyikazi wake wamepata mafunzo kuhusu usimamizi na uendeleshaji wa vipindi.

Iwapo stesheni hiyo itakaidi maagizo ya CAK basi shirika hilo halitakuwa na budi kuchukua hatua zaidi ikiwemo kuwapokonya leseni yao.

CAK imeagiza vituo vyote vya utangazaji kuzingatia kanuni zilizowekwa kulingana na sheria.