Jamaa atiwa mbaroni kwa kunajisi mtoto wa sekondari Bomet

Muhtasari

•Polisi walimfumania Belamy Kirui 27, katika chumba kimoja cha kulala cha Lembus ambapo anadaiwa kuchovya asali ya msichana huyo mwenye umri wa miaka 16.

Pingu
Image: Radio Jambo

Polisi katika kaunti ya Bomet wanamzuilia jamaa mmoja anayedaiwa kunajisi mtoto wa sekondari katika eneo la Chebole, Kaunti ndogo ya Sotik.

Polisi walimfumania Belamy Kirui 27, katika chumba kimoja cha kulala cha Lembus ambapo anadaiwa kuchovya asali ya msichana huyo mwenye umri wa miaka 16.

Maafisa wa DCI wameripoti polisi walifika katika eneo la tukio baada ya kupokeaa ripoti kutoka kwa mzee aliyepata ufahamu kuhusu kitendo hicho cha aibu.

Walipofika pale katika vyumba vile vya kulala waliamrisha mshukiwa kufungua mlango kwani ulikuwa umefungwa kutoka ndani.

Umma uliokuwa umejawa na ghadhabu ulikuwa umemsubiri mshukiwa nje ya vyumba hivyo tayari kumfunza adabu ila polisi wakaokoa maisha yake.

Mshukiwa pamoja na mhasiriwa walipelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi na baada ya hapo mshukiwa akawekwa kizuizini akisubiri kufikishwa mahakamani.