Rais Joe Biden ateua balozi mpya wa Kenya

Muhtasari

• Rais wa Marekani Joe Biden amemteua aliyekuwa Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Hewlett Packard (HP) na rais Meg Whitman kuwa balozi wa Marekani nchini Kenya. 

• Aligombea ugavana wa jimbo la California mwaka wa 2010 kwa chama cha Republican lakini akashindwa na mgombea wa Democrat Jerry Brown. 

• Alimuunga mkono seneta wa sasa Mitt Romney akigombea urais mwaka wa 2008.

Image: GETTY IMAGES

Rais wa Marekani Joe Biden amemteua aliyekuwa Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Hewlett Packard (HP) na rais Meg Whitman kuwa balozi wa Marekani nchini Kenya. 

Anatarajiwa kuchukua nafasi ya balozi Kyle McCarter aliyeondoka Januari 2021. Margaret C. Whitman (Meg), mkurugenzi mkuu wa biashara na mgombea wa zamani wa Gavana wa California, ni Mjumbe wa Bodi ya Procter and Gamble na General Motors, na Mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa katika shirika la Teach for America, Ikulu ya White House ilisema katika ujumbe wake. 

Whitman alitumia miongo kadhaa katika majukumu ya kiwango cha juu katika mashirika mbali mbali, lakini pia amekuwa katika siasa kwa miaka mingi. 

Aligombea ugavana wa jimbo la California mwaka wa 2010 kwa chama cha Republican lakini akashindwa na mgombea wa Democrat Jerry Brown. 

Alimuunga mkono seneta wa sasa Mitt Romney akigombea urais mwaka wa 2008 - kabla ya hatimaye kuwa mwenyekiti mwenza wa kampeni ya kitaifa ya Seneta John McCain mwaka wa 2012.  

Alimuunga mkono Hillary Clinton wa Democrat katika kinyang'anyiro cha 2016 dhidi ya Donald Trump.