COVID- 19: Wagonjwa wapya 3, 297; Vifo 8 vyaripotiwa

Muhtasari

•Kwa sasa wagonjwa 835 wamelazwa hospitalini huku wengine 21, 692 wakipokea matibabu kutoka nyumbani. Wagonjwa 39 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Wizara ya afya nchini imetangaza visa vipya 3, 297 vya waathiriwa wa Covid-19.

Kiwango cha maambukizi kwa sasa ni 34,2% huku jumla ya visa vilivyowahi kuripotiwa hapa nchini sasa ikifika  288, 951.

Sampuli 9, 637 ziliweza kupimwa katika kipindi cha masaa 24 ambacho kimepita. Mtoto wa mwezi mmoja mpya ndiye mgonjwa mdogo zaidi huku mzee zaidi akiwa mkongwe wa miaka 101.

Kaunti ya Nairobi imeripoti visa 982, Makueni visa 233, Siaya 226, Nakuru 115, Kakamega 114, Migori 114, Machakos 110 huku kaunti zingine zikiripoti visa chini ya 100.

Wagonjwa 236 wameweza kupata afueni, 63 ambao walikuwa wamelazwa hospitalini huku 236 wakipona kutoa manyumbani.

Habari za kusikitisha ni kwamba vifo 8 kutokana na maradhi hayo vimeripotiwa. Jumla ya vifo vya Corona sasa imefika 5, 372.

Kwa sasa wagonjwa 835 wamelazwa hospitalini huku wengine 21, 692 wakipokea matibabu kutoka nyumbani. Wagonjwa 39 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Watu 5, 704, 996 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 4, 018, 791 kati yao wakiwa wamepokea dozi zote mbili.