Mchimba dhahabu aokolewa baada kukwama kwenye machimbo yaliporomoka kwa siku tatu

Alinaswa baada ya kuta za mgodi kuporomoka.

Muhtasari

•Noah Ogweno aliokolewa Jumapili, siku tatu baada ya mkasa huo uliotokea adhuhuri ya  Alhamisi. 

Migodi ya Kopuodho ambapo Noah Ogweno aliokolewa
Migodi ya Kopuodho ambapo Noah Ogweno aliokolewa
Image: MANUEL ODENY

Furaha isiydhibitika ilitanda katika machimbo ya dhahabu ya Kopuodho yaliyo eneo la Rongo baada ya mchimba mgodi aliyekuwa amezikwa chini ya ardi kwa siku tatu kuokolewa akiwa hai.

Noah Ogweno aliokolewa Jumapili, siku tatu baada ya mkasa huo uliotokea adhuhuri ya  Alhamisi. Alinaswa baada ya kuta za mgodi  kuporomoka.

Juhudi za pamoja za wenzake na viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na Mbunge wa eneo hilo Paul Abuor ambaye alitoa trekta ya kuchimba zilizaa matunda hatimaye. Hii ilikuwa baada ya mikesha mitatu ya usiku.

"Tunawashukuru waendeshaji trekta na waokoaji wengine ambao walifanya kazi usiku na mchana. Pia ningependa kuwashukuru wote waliotupatia msaada katika kipindi chote cha operesheni hii ya kuokoa maisha ya Noah,” Abuor alisema jana.

Ogweno aliokolewa na kukimbizwa katika hospitali ya misheni ya Tabaka iliyo kaunti ya Kisii.

Jacob Migoga ambaye ni mchimbaji dhahabu huko Rongo aliiomba serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo wa dhahabu waweze kufanya kazi katika  mazingira  salama.

Gavana wa Migori Okoth Obado alisema serikali ya kaunti ilichukua hatua haraka kumwokoa Ogweno baada ya kupokea habari kuhusu mkasa huo.

"Tuliomba kwamba vifaa vyetu vipate kufika mahali alipokuwa amenaswa. Tulikuwa na matumaini kwamba tungewezakumpata akiwa hai kwa sababu alikuwa akiwasiliana nasi,” Obado alisema.

Gavana huyo alisema waliomba usaidizi zaidi ili kuweza kuvunja miamba migumu ambayo ilizuia trekta ya kuchimba.

Aliwaomba wadau kuja kusaidia wachimbaji madini, akisema sekta hiyo inapaswa kuungwa mkono.

(Utafsiri: Samuel Maina)