Omtatah awasilisha ombi la kumzuia Ruto kugombea kiti cha urais

Muhtasari
  • Katika ombi alilowasirisha, Jumatatu alitaka afisa yeyote wa umma, waondoke katika nyadhifa ambazo wameshikilia
okiya omtata
okiya omtata
Image: Maktaba

Mwanaharakati Okiya Omtata ameenda kortini  akitaka Raibu Rais William Ruto  kuzuiliwa kugombea kiti cha urais. 

Katika ombi alilowasirisha, Jumatatu alitaka afisa yeyote wa umma, waondoke katika nyadhifa ambazo wameshikilia kabla ya kukubaliwa na kugombea kiti chochote nchini.

Katika ombi lake anaowataka wazuiliwe kugombea kiti  ni; naibu rais aliyemamlakani, gavana aliyeofisini na pia naibu wake, wabunge wa viti maalum na MCA walio kwenye uongozi

"Tamko kwamba rais aliyemamlakani  naibu wa rais, Magavana walio uongozini pia ,naibu gavana hawawezi kuchaguliwa kwa nafasi za uongozi isipokuwa zile wameshikilia, " alisema Okiya Omtata.

Omtatah aliongeza kuwa sheria itolewe kwamba rais aliyemadarakani, naibu rais, gavana na manaibu wake lazima waondoke afisini kabla ya kuchaguliwa kwa nyadhifa tofauti na zioe wanazoshilikia kwa sasa.

Kampeni rasmi za uchaguzi mkuu wa 2022 zitaanza Mei 10 baada ya wagombeaji urais Kampeni Rasmi za Uchaguzi Mkuu wa 2022 zitaanza Mei 10 baada ya wagombeaji urais kuwasilisha karatasi zao kwa IEBC, hadi Agosti 6, siku mbili hadi siku ya kupiga kura.

Tume ya uchaguzi ilifichua ratiba ya uchaguzi wa 2022, na kuwataka watumishi wa umma wanaotaka kugombea wadhifa huo kujiuzulu ifikapo Februari 9, mwaka ujao.