Tanzia:Esther Passaris ampoteza baba yake

Muhtasari
  • Passaris alimuelezea baba yake mwenye umri wa miaka 79 kama mume mwenye upendo, baba wa ajabu na Papou (babu)
Esther Passaris
Image: Hisani

Mwakilishi wa Wanawake wa Nairobi Esther Passaris yuko katika maombolezo kufuatia kifo cha babake, ambacho alitangaza kwenye mitandao ya kijamii Ijumaa usiku.

Passaris alimuelezea baba yake mwenye umri wa miaka 79 kama mume mwenye upendo, baba wa ajabu na Papou (babu).

"Sehemu yangu imekufa leo. Mbingu zilifunguka na kumaliza mateso ya baba yangu,Baba yangu ni mbunifu wa majini kitaaluma, alipata mafanikio mengi katika miaka yake 79. Kuanzia kujenga meli ya kwanza nchini Kenya, MV Mwewe, hadi kufundisha na kuwashauri vijana wa Ngome Football Club huko Mombasa," Aliandika Passaris.

Katika chapisho lingine alisema;

"Baba alifanya kazi katika kampuni ya Southern Engineering Company Limited, COMARCO, kabla ya kujumuisha HELMACO, ambayo aliiongoza hadi kustaafu. Lakini ukiangalia nyuma, hakuna mafanikio yake yoyote yanayolinganishwa kwa mwanafamilia ambaye alikuwa…”

Passaris aliomboleza babake kama mtu anayemcha Mungu ambaye aliomba ulinzi juu ya familia na nchi yake.

"Ingawa nimeumia moyoni, roho yangu iko vizuri," alisema.