Covid-19:Watu 170 wapatikana na corona,556 wapona,4 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 4 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,558
  • Kuna wagonjwa 721 ambao wamelazwa hospitalini, 5,733 wamejitenga nyumbani
  • Vile vile kuna wagonjwa 40 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
  • Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 11,553,637
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe akutana na Baraza la Magavana mjini Mombasa mnamo Desemba 15.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe akutana na Baraza la Magavana mjini Mombasa mnamo Desemba 15.
Image: MAGDALINE SAYA

Visa 170 vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 3,659 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 143 ni wakenya huku 27 wakiwa raia wa kigeni,86 ni wanaume huku 84 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 320,399 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 4.7%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,189,945.

Vile vile watu 556 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 291,917, 506 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 50 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 4 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,558.

Kuna wagonjwa 721 ambao wamelazwa hospitalini, 5,733 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 40 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 11,553,637.