IPOA kuchunguza kuhusika kwa polisi katika siri ya miili ya Yala

Muhtasari
  • IPOA kuchunguza kuhusika kwa polisi katika siri ya miili ya Yala
  • Katika taarifa mnamo Ijumaa, mwenyekiti wa Ipoa Anne Makori alisema uchunguzi ulianza Januari 25
Anne Makori mwneyekiti wa IPOA
Anne Makori mwneyekiti wa IPOA

Makori aliwahakikishia Wakenya kwamba Ipoa inasalia kujitolea kuwa huru, kutopendelea na kuwa na haki.

"Baada ya kukamilika kwa upelelezi wote wawili, ambapo kosa litapatikana, mamlaka haitasita kutoa mapendekezo, ikiwa ni pamoja na lakini sio tu kwa mashtaka."

 

 

 

Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi inatazamiwa kuchunguza ikiwa kulikuwa na polisi waliohusika katika vifo vya watu ambao miili yao iliopolewa kutoka River Yala.

Katika taarifa mnamo Ijumaa, mwenyekiti wa Ipoa Anne Makori alisema uchunguzi ulianza Januari 25.

"Kama sehemu ya uchunguzi kubaini kama polisi walihusika katika kifo chochote, timu ilihudhuria uchunguzi wote wa uchunguzi wa maiti na kwa sasa inaendelea na uchunguzi wa kina," Makori alisema.

Katika kesi nyingine, mamlaka hiyo inachunguza kifo cha Duncan Okoko anayedaiwa kufariki akiwa mikononi mwa polisi Januari 22.

Kulingana na Ipoa, Okoko alikuwa ameenda kufuatilia suala katika kituo cha polisi.

Kufuatia ripoti za kifo chake, Ipoa ilituma timu ya majibu ya haraka mnamo Januari 23 kukusanya habari ambazo zitakuwa muhimu katika hali ya ufichuzi kuhusu kifo cha Okoko.

"Timu ilihudhuria uchunguzi wake wa maiti asubuhi ya leo (Ijumaa)."