Askari kukosa kuzikwa kijeshi baada ya kujitoa uhai.

Muhtasari
  •  Jeshi la polisi la Tanzania limesema kwamba askarai aliyejiua kwa kujitoa uhai hatozikwa kwa kanuni za kijeshi
  • Grayson Mahembe alijitoa uhai mkoani Mtwara akiwa mahabusu ya peke yake ambayo aliwekwa kufuatia tuhuma za mauaji ya mfanyibiashara wa madini
instagram KWA HISANI
Image: millard ayo

Jeshi la polisi la Tanzania limesema kwamba askari aliyejiua kwa kujitoa uhai hatozikwa kwa kanuni za kijeshi.

“Kuhusu mazishi yake, askari anayefariki kwa kujitoa uhai hazikwi kijeshi, hakuna gwaride la mazishi n risasi au mabomu ya kishindo kwani anahesabiwa kuwa hajafa kishujaa na hastahili heshima hiyo,” alisema mkuu huyo wa polisi.

Akizungumza na vyombo vya habari Jumatatu 31/01/2022, mmoja wa wakuu wa polisi amesema kwamba , kumeshuhudiwa upotoshaji kuhusiana na tukio hilo huku akisema kwamba askari huyo, Grayson Mahembe alijitoa uhai mkoani Mtwara akiwa mahabusu ya peke yake ambayo aliwekwa kufuatia tuhuma za mauaji ya mfanyibiashara wa madini.

Wananchi wameonekana kuchanganyikiwa kwa taarifa hii huku wakiomba jeshi la polisi kwa ushirikiano wa serikali kuu kumzika Mahembe kwa heshima za jeshi la Tanzania, huku wakisubiria uchunguzi zaidi kufanywa ili kujua kisa hicho kilitokea vipi.