Ezekiel Mutua ateuliwa kuwa bosi mpya wa MCSK

Muhtasari
  • Ezekiel Mutua ateuliwa kuwa bosi mpya wa MCSK
Ezekiel Mutua
Image: Maktaba

Aliyekuwa bosi wa Bodi ya Uainishaji wa Filamu nchini (KFCB) Dkt. Ezekiel Mutua ametawazwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Chama cha Hakimiliki ya Muziki Kenya (MCSK).

Uteuzi huo ulitangazwa na Mwenyekiti wa Bodi ya MCSK Lazarus Muli kupitia taarifa Jumatatu, ambaye alibainisha kuwa Dkt Mutua ndiye bosi wa jumuiya hiyo kuanzia Ijumaa, Machi 25.

“ Uteuzi wa Mutua unafuatia mahojiano makali ya ushindani ambapo aliibuka kinara kati ya wagombeaji waliohojiwa kuwania nafasi hiyo,” alisema Muli.

Mutua alikuwa, hadi Agosti mwaka jana, katika usukani wa KFCB, ambapo alijipatia lebo ya ‘polisi wa maadili’ wa Kenya kwa ukosoaji wa kuwa na maadili ya hali ya juu.

Mara nyingi alikuwa akizozana na waundaji maudhui wa Kenya, ambao mara kwa mara walilalamika kuhusu udhibiti wa bodi tangu alipochukua hatamu mwaka wa 2015.

Huku akizungumza baada ya uteuzi huo Mutua alisema kwamba anafuraha kujiunga na tasnia burudani na wala sio kama mkuu wala kama mtetezi wa haki za wasanii.