Serikali yachukuwa hatua kali dhidi ya kampuni za mafuta kwa kusababisha uhaba

Muhtasari

• Waziri alisema kwamba kunahifadhi ya kutosha ya mafuta nchini.

• Juma alishtumu vikali baadhi ya kampuni za mafuta nchini kwa kusababisha uhaba wa bidhaa ya mafuta nchini makusudi kwa manufaa yao ya binafsi.

Waziri wa ulinzi Monica Juma
Waziri wa ulinzi Monica Juma
Image: DOUGLAS OKIDDY

Serikali imetangaza kuwachukulia hatua kali wafanyibiashara wa mafuta waliosababisha uhaba wa bidhaa hiyo nchini makusudi.

Akihutubia mkao wa wanahabari siku ya Alhamisi Kaimu waziri wa kawi Monica Juma pia aliwahakikishia wakenya kuwa mikakati imewekwa kuhakikisha kuwa hali ya kawaida inarejea katika muda wa saa 72.

Waziri alisema kwamba kunahifadhi ya kutosha ya mafuta nchini.

Alitowa wito kwa wananchi kuwa watulivu huku swala hilo likishughulikiwa.

Juma alishtumu vikali baadhi ya kampuni za mafuta nchini kwa kusababisha uhaba wa bidhaa ya mafuta nchini makusudi kwa manufaa yao ya binafsi.

 Waziri alisema alithibitisha kuwa nchi ina akiba ya mafuta ya kutosha ingawa alishtumu baadhi ya kampuni kwa kuficha mafuta na kuelekeza mgao wa mafuta yaliyonuiwa kwa soko la Kenya hadi nchi zingine katika kanda hii.

Alisema kuwa Mamlaka ya Nishati na Petroli na Udhibiti wa nishati tayari imetoa barua za kuonya kampuni za mafuta ili kusubiri kupandishwa kwa bei za bei katika bei mpya za kila mwezi.

Wenye magari pia wamehimizwa kuepuka kununua kiasi kikubwa cha mafuta ili kuepusha mzozo zaidi.