Uchumi wa Kenya uliboreka kwa asilimia 7.5 mwaka 2021

Muhtasari

• Hii ni baada ya kudorora kwa asilimia 0.3 mwaka 2020, kutokana na athari za janga la Covid-19. 

• Gharama ya maisha hata hivyo iliongezeka kwa kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha miaka 4 kwa asilimia 6.1% mwaka 2021.

• Sekta ya usafiri ilirekodi kiwango cha juu zaidi cha mfumuko wa bei cha 12.3% kutokana na kuongezeka kwa bei za petroli na dizeli.

Pesa za Kenya
Pesa za Kenya
Image: HISANI

 Uchumi wa Kenya ulikua kwa asilimia 7.5 mwaka wa 2021, kulingana na utafiti wa Kiuchumi wa mwaka 2022 uliofanya shirika la Kitaifa ya Takwimu. 

Hii ni baada ya kudorora kwa asilimia 0.3 mwaka 2020, kutokana na athari za janga la Covid-19. 

Ukuaji wa mwaka jana ulichangiwa zaidi na sekta ya viwanda, uuzaji wa jumla na reja reja, usafiri na uhifadhi na sekta ya hoteli na huduma, huku shughuli za usafiri zikirejelea. 

Elimu na shughuli za kifedha na bima pia zilichukua jukumu kubwa katika kukuza ukuaji. 

"Shughuli zote za kiuchumi zilisajili ukuaji mzuri zaidi isipokuwa kilimo," mkurugenzi mkuu wa KNBS Mcdonald Obudho alisema wakati wa kutolewa kwa utafiti huo, mjini Nairobi, Alhamisi. 

Gharama ya maisha hata hivyo iliongezeka kwa kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha miaka 4 kwa asilimia 6.1% mwaka 2021 Wananchi walikuwa na wakati mgumu mwaka 2021 kwani walilazimika kuingia zaidi ndani ya mifuko yao ili kumudu mahitaji ya kimsingi. 

Kulingana na Utafiti wa Uchumi wa 2022 uliotolewa Alhamisi, mfumuko wa bei ulipanda hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 5.4 mwaka uliopita. 

Hii ilikuwa gharama ya juu zaidi ya maisha iliyorekodiwa nchini tangu 2017 ilipofikia asilimia nane. 

Ongezeko hilo limechangiwa zaidi na kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa za vyakula. 

Sekta ya usafiri ilirekodi kiwango cha juu zaidi cha mfumuko wa bei cha 12.3% kutokana na kuongezeka kwa bei za petroli na dizeli.