4 waaga dunia katika ajali ya barabarani Machakos

Naibu kamanda wa polisi wa Machakos Mose Nthiwa alisema waliofariki ni pamoja na watu wazima watatu na mtoto mmoja.

Muhtasari
  • Nthiwa alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Kithini katika kaunti ndogo ya Machakos mnamo Jumatano
  • Alisema baadhi ya waliokuwemo walipatiwa matibabu katika hospitali hiyo na kuruhusiwa wakiwa katika hali nzuri
4 waaga dunia katika ajali ya barabarani Machakos
Image: GEORGE OWITI

Watu wanne wamefariki katika ajali ya barabarani katika kaunti ya Machakos.

Naibu kamanda wa polisi wa Machakos Mose Nthiwa alisema waliofariki ni pamoja na watu wazima watatu na mtoto mmoja.

Nthiwa alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Kithini katika kaunti ndogo ya Machakos mnamo Jumatano.

Bosi huyo wa polisi alisema gari hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi, lilikuwa na abiria kumi na saba wakati wa tukio hilo.

4 waaga dunia katika ajali ya barabarani Machakos
Image: GEORGE OWITI

"Leo asubuhi saa 09.30 katika eneo la Kithini kando ya barabara ya Nairobi - Machakos. Walijumuisha abiria 14 na watoto watatu. Gari lilipoteza udhibiti na kupinduka. Abiria watatu, wote wazima walikufa papo hapo huku mtoto mmoja akipoteza maisha katika Hospitali ya Machakos Level 5. ," Nthiwa alisema.

Nthiwa alisema majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Machakos Level 5.

Alisema baadhi ya waliokuwemo walipatiwa matibabu katika hospitali hiyo na kuruhusiwa wakiwa katika hali nzuri.

Image: GEORGE OWITI

Nthiwa alisema mabaki ya gari hilo lililoharibika kwa kiasi kikubwa yalivutwa hadi kituo cha polisi cha Machakos yakisubiri kufanyiwa ukaguzi huku miili ikitolewa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo hiyo.

Alitoa wito kwa madereva wa magari kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima.

Nthiwa alisema madereva wa magari wanapaswa kuzingatia sheria na kanuni za barabarani