Kifaa kinachoshukiwa kuwa bomu chapatikana jijini Nairobi

Kifaa hicho kilionekana na wapita njia asubuhi ya Jumatano.

Muhtasari

•Barabara ya Taveta Lane imezingirwa na maafisa wa polisi kwa sababu za kiusalama.

Crime Scene

Kifaa kinachoshukiwa kuwa cha kilipuzi kimepatikana nje ya Ebony House, katika kijibarabara cha Taveta, karibu Tom Mboya Street jijini Nairobi.

Barabara hiyo imezingirwa na maafisa wa polisi kwa sababu za kiusalama. 

Kundi kubwa  la watazamaji wenye shauku wamekuwa wakifuatilia eneo la tukio kwa mbali. Waandishi wa habari pia wapo kwenye eneo la tukio kufuatilia yanayojiri.

Kifaa hicho kilionekana na wapita njia asubuhi ya Jumatano. Kilikuwa kimeachwa katika eneo linalopita maji machafu.

Polisi wanasema wanasubiri timu ya wataalamu wa mabomu kufika eneo la tukio ili kukagua kifaa hicho.