Wakili Miguna afichua siku atakayo wasili nchini

Hii ilikuwa mara yake ya pili kutolewa nje ya nchi hadi Kanada, nchi ambayo pia ana uraia halali.

Muhtasari
  • Wakili huyo alifichua hayo Jumatano akisema sasa atasafiri kurejea Kenya Oktoba 20
  • Alidai kuhamishwa kwa nguvu hadi Kanada mnamo Machi 28, 2018
Image: TWITTER// MIGUNA MIGUNA

Serikali imeondoa arifa nyekundu zilizowekwa kwa wakili Miguna Miguna mnamo Machi 2018.

Wakili huyo alifichua hayo Jumatano akisema sasa atasafiri kurejea Kenya Oktoba 20.

“Serikali ya William Ruto na Rigathi Gachagua imeondoa Arifa Nyekundu zilizowekwa dhidi yangu na Uhuru Kenyatta kinyume cha sheria na ushirikiano wa Raila Odinga.

"Kuwasili kwangu: Oktoba 20 saa kumi na mbili asubuhi. Sheria ya sheria, kutoogopa, kuendelea na kuzingatia vimetawala," Miguna alisema kwenye ukurasa wake wa twitter.

Kuondolewa kwa marufuku ya kusafiri sasa kunamaliza kusubiri kwa zaidi ya miaka mitatu kwa wakili huyo kurejea nyumbani baada ya kufukuzwa kwa nguvu hadi Kanada mnamo Machi 2018.

Mnamo Septemba 13, Miguna alidai kuwa arifa hizo nyekundu zingeondolewa siku moja baadaye lakini hazikutimia.

Aliwaambia Wakenya kwamba Rais William Ruto alikuwa amemhakikishia kurejea kwake mara tu arifa hizo nyekundu zitakapoondolewa.

"Baadaye, nitafanyiwa upya Pasipoti yangu ya Kenya na nitatangaza tarehe ya kurejea katika nchi yangu," alisema.

Alidai kuhamishwa kwa nguvu hadi Kanada mnamo Machi 28, 2018.

"Niliburuzwa, kushambuliwa, kuleweshwa  na kusafirishwa kwa nguvu hadi Dubai," Miguna aliandika katika chapisho la Facebook.

Hii ilikuwa mara yake ya pili kutolewa nje ya nchi hadi Kanada, nchi ambayo pia ana uraia halali.

Serikali ilisisitiza kuwa yeye si raia wa Kenya.