Natembeya akutana na muuguzi aliyemchezea densi mtoto mgonjwa

Natembeya aliahidi kumlipia ada ya shule mwanafunzi huyo.

Muhtasari
  • Natembeya alimkaribisha Elizabeth Robai Lukelesia Jumanne jioni katika ofisi yake katika makao makuu ya kaunti ya Trans Nzoia ili kumshukuru rasmi kwa ishara yake
GAVANA NATEMBEYA NA MUUGUZI ELIZABETH
Image: TWITTER

Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya amemsifu muuguzi wa Chuo cha Mafunzo ya Udaktari cha Kenya (KMTC) ambaye amevumaa mitandaoni kwa kumtumbuiza mtoto mgonjwa katika wadi.

Natembeya alimkaribisha Elizabeth Robai Lukelesia Jumanne jioni katika ofisi yake katika makao makuu ya kaunti ya Trans Nzoia ili kumshukuru rasmi kwa ishara yake.

"Niliweza kukutana na muuguzi wa watoto Robai Elizabeth Lukelesia jioni hii. Muuguzi aliyejitolea anayehudumu kwa bidii."

Natembeya aliahidi kumlipia ada ya shule mwanafunzi huyo.

"Nimeahidi kumlipia ada ya masomo kwa muda uliosalia wa masomo yake, zaidi kuhakikisha anapata mafunzo ya kazi na hatimaye kufyonzwa ili kuhudumu kama muuguzi wa watoto.

Hongera Elizabeth Robai juhudi na kujitolea kwako vimezaa matunda,"Natembeya Alisema.