Maafisa wa vikosi maalum vya polisi wakiwemo RDU kushika doria jijini Nairobi

Baraza la mawaziri lilikiri kuongezeka kwa visa vya utovu wa usalama katika jiji la Nairobi

Muhtasari

• Wananchi wengi wameripoti kuhangaishwa na magenge ya majambazi katika mwa jiji la Nairobi na vyiungani mwake.

Naibu Rais William Ruto na maafisa wa AP katika makazi ya Naibu Rais Karen mnamo Agosti 30, 2021.
Naibu Rais William Ruto na maafisa wa AP katika makazi ya Naibu Rais Karen mnamo Agosti 30, 2021.
Image: STAR

Ili kukabiliana na utovu wa usalama katika jiji la Nairobi baraza la mawaziri limeidhinisha matumizi wa vikosi maalum vya polisi kushika doria ili kukabiliana na magenge ambaye yamekuwa hakiwahangaisha wananchi wa jiji la Nairobi.

Katika mkutano wa baraza la mawaziri uliyoandaliwa siku ya Jumanne katika ikulu ya Nairobi chini ya uwenyekiti wa rais William Ruto, baraza la mawaziri lilikiri kuongezeka kwa visa vya utovu wa usalama katika jiji la Nairobi na kutaja umuhimu wa kuimarisha doria ili kukabili vijana watovu.

“Ilibainika kuwa usimamizi wa usalama wa Kaunti ya Nairobi ulikuwa umefanyiwa mabadiliko ili kuimarishwa zaidi na kutumwa kwa vitengo maalum vya polisi kutoka kwa Kitengo cha Huduma ya Jumla na Kitengo cha dharura (RDU),” taarifa ya baraza la mawaziri ilisema.

Hatua hii inajiri huku kukiwa na tetesi kuwa kuzorota kwa usalama katika jiji la Nairobi na maeneo mengine mengi ya nchi kunatokana na hatua ya baadhi ya viongozi wa serikali kukashifu maafisa wa polisi kutokana na utendakazi wao.

Kumekuwepo fununu kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa baadhi ya maafisa wa polisi waliokuwa wakihudumu katika idara ya DCI kwa madai ya mauaji ya kiholela huenda kuliibua tumbo joto miongoni mwa polisi na kuwa na hofu ya kuwakabili wahalifu ifaavyo.

Hata hivyo katika mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Jumanne serikali ilipongeza mchango wa idara ya polisi katika kudumisha usalama nchini na kutaka idara hiyo kuendeleza kazi nzuri ili kuhakikisha kila mwananchi yuko salama popote pale alipo.

 “Baraza la Mawaziri limewapongeza maafisa wetu wa usalama wanaoendelea kujitolea sana kuweka taifa letu na mipaka yake salama”, taarifa hiyo iliyongeza.

Wananchi wengi wameripoti kuhangaishwa na magenge ya majambazi katika mwa jiji la Nairobi na vyiungani mwake. Visa vya utovu wa usalama pia vimeripotiwa kuongezeka katika maeneo kadhaa ya nchi.