Kenya Power yapendekeza kuongeza ada za umeme

Mabadiliko yatawafanya watumiaji kupokea karibu nusu ya tokeni wanazopokea kwa sasa kwa malipo sawa.

Muhtasari

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta alikuwa amepunguza gharama ya umme mwaka 2022 ikiwa moja wapo wa mikakati aliyokuwa ameweka kupunguza gharama ya maisha. 

Kenya Power

Kampuni ya kusambaza umeme nchini Kenya Power imependekeza kuongeza ada za umeme hatua ambayo imezua tumbo joto miongoni mwa wananchi hasa katika sekta ya jua kali ambao wanakabiliwa na kupanda kwa gharama ya maisha.

Katika pendekezo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA), Kenya Power inataka kuongeza mapato ili kukidhi majukumu ya kimkataba ya ununuzi wa umeme na kuafiki gharama za usambazaji umeme ambazo imesema zimeongezeka marudufu.

Mabadiliko yaliyopendekezwa yanaweza kuwafanya watumiaji kupokea karibu nusu ya tokeni wanazopokea kwa sasa kwa malipo sawa.

Kenya Power inapendekeza kuondoa vitengo vya watumiaji wengi na kuweka tu kiwango kimoja, kwa watumiaji wote wanaotumia zaidi ya uniti 30 kwa mwezi. Watalipa Ksh.21.68 kwa kila uniti.

Rais William Ruto alikuwa ameahidi kupunguza gharama za umeme alipochukuwa mamlaka na pendekezo hili jipya linakwenda kinyume na ahadi yake.   

Mteja mjini Loresho, Nairobi, akiweka funguo kwenye kisanduku cha mita mnamo Aprili 25, 2018. /ENOS TECHE
Mteja mjini Loresho, Nairobi, akiweka funguo kwenye kisanduku cha mita mnamo Aprili 25, 2018. /ENOS TECHE

Rais mtaafu Uhuru Kenyatta alikuwa amepunguza gharama ya umme mwaka 2022 ikiwa moja wapo wa mikakati aliyokuwa ameweka kupunguza gharama ya maisha. 

Mteja wa kitengo cha P kwa shilingi 1,500 alikuwa anapata 58.9 mnamo Desemba 2021, lakini kufuatia kupunguzwa kwa bei kutokana na ruzuku ya umeme iliyoletwa na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta, kiasi kama hicho kilimnufaisha mteja kwa uniti 68.6 mnamo Januari 2022, hadi Septemba 2022. Gharama za umeme hata hivyo zilipanda mara moja na zimekuwa zikipanda kila mara.