Mshukiwa wa mauaji ya wakili Willie Kimani ahukumiwa kifo

Mshtakiwa wa tatu, kwa upande mwingine, atatumikia kifungo cha miaka 24 jela huku mtoa taarifa wa polisi akihukumiwa miaka 20.

Muhtasari
  • Mahakama ilisema kwamba ilizingatia kwamba Sylvia Wanjiru ndiye aliyekuwa mhusika mdogo zaidi katika kundi hilo.
Image: Enos Teche

Fredrick ole Leliman, afisa wa polisi ambaye alikuwa mshukiwa mkuu na ambaye alipanga mauaji ya kikatili ya Wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwenda na dereva Joseph Muiruri amehukumiwa kifo.

Maafisa  wanne, Fredrick Leliman (mshukiwa mkuu), Stephen Cheburet, na Sylvia Wanjiku, na mtoa habari Peter Ngugi, ambao walishtakiwa kwa mauaji ya wakili wa Nairobi Willie Kimani, walihukumiwa siku ya Ijumaa.

Katika uamuzi wake wa Ijumaa, Februari 3, Hakimu Jessie Lesit alimhukumu Leliman kifo huku mshtakiwa wa pili akipokea miaka 30 jela.

Mshtakiwa wa tatu, kwa upande mwingine, atatumikia kifungo cha miaka 24 jela huku mtoa taarifa wa polisi akihukumiwa miaka 20.

"Mshtakiwa wa kwanza anahukumiwa kifo katika kila moja ya makosa matatu, mshtakiwa wa pili anahukumiwa kifungo cha miaka thelathini, mshtakiwa wa tatu anahukumiwa miaka 24 na mshtakiwa wa tano anahukumiwa kifungo cha miaka ishirini," Jaji Jessie Lesit alisema.

Mahakama ilisema kwamba ilizingatia kwamba Sylvia Wanjiru ndiye aliyekuwa mdogo zaidi katika kundi hilo na alikuwa mdogo wakati wa uhalifu.