Mwili wa Jeff Mwathi umefukuliwa Ijumaa

Jeff Mwathi alizikwa tarehe 3, Machi katika Kaunti ya Nakuru

Muhtasari

• Ripoti za hapo awali zilidai kuwa Jeff Mwathi aliuawa wala hakuanguka kutoka ghorofani.

Jeff Mwathi, aliyefariki kwa utata nyumbani kwa DJ Fatxo
Jeff Mwathi, aliyefariki kwa utata nyumbani kwa DJ Fatxo
Image: Facebook//Simon Mwangi Muthiora

Shughuli ya ufukuzi wa mwili wa Jeff Mwathi umefukuliwa katika zoezi lililoendeshwa na maafisa wa idara ya uhalifu wa jinai.

Mwili huo ulifukuliwa kwa ajili ya uchunguzi kubiani kilichosababisha kifo chake. Uchunguzi utafanywa kisha baadaye mwili wake utazikwa tena.

Mkurugenzi wa DCI Amin Mohammed alitoa tangazo hilo alipoandamana na wachunguzi hadi Redwood Apartments ambapo Jeff Mwathi alifariki baada ya kuanguka kutoka kwenye jengo hilo. Hatua hiyo ilikuja baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa DNA na Toxicology.

Amin  na maafisa wake wanatathmini  upya eneo la uhalifu ambapo Jeff aliripotiwa kufariki akiwa nyumbani kwa msanii maarufu wa Kikuyu DJ Fatxo.

"Katika shughuli hiyo, timu ya Makao Makuu ya DCI na wafanyikazi wa Eneo la Uhalifu kutoka Maabara ya Kitaifa ya Uchunguzi wa Kitaifa ya DCI walitafuta kutambua mapungufu ambayo uchimbaji wa kaburi unatarajiwa kutoa majibu mara moja," DCI ilisema.

Mohamed anataka uchunguzi wa tukio hilo ufanywe haraka ili kubaini kama kulikuwa na mchezo usio wa kawaida katika kifo cha Mwathi. Mnamo Februari 22, mwathiriwa alidaiwa kuanguka kutoka kwenye dirisha la ghorofa ya 10 la jumba la Redwood kwake DJ Fatxo, jina halisi Lawrence Njuguna alipokuwa akiburudika  na marafiki zake.

Ripoti zinaonyesha kuwa Mwathi alikutana na mtumbuizaji huyo saa chache mapema ili kufanya majadiliano kuhusu tamasha la usanifu wa ndani ambalo DJ Fatxo alitaka afanye kwa ada. Aliwahakikishia wananchi kuwa uchunguzi huo uafanywa kwa umakinifu na hakuna mahali ambapo pataachwa na mwanya.

Samidoh mehudhuria shughuli hiyo ya ufukuzi.