#RHONAIROBI

#RHONairobi: Ndani ya maisha ya kifahari ya wanawake mashuhuri wa Kenya

Muhtasari
  • Ukiwa na Showmax, unaweza kutazama chochote unachotaka, wakati wowote, mahali popote kwenye Programu ya Showmax au tovuti ya Showmax.
  • #RHONairobi inashirikisha wanawake wasita warembo na wenye maono makubwa katika maisha yao ya kifahari, mahusiano yao na kazi zao ndani ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Real Housewives of Nairobi ni sinema ya uhalisia ya kusisimua ambayo huwaonyesha watazamaji wake maisha ya wanawake wa tabaka la juu wa Nairobi. Kipindi hiki kinashirikisha wanawake wasita warembo na wenye maono makubwa katika maisha yao ya kifahari, mahusiano yao na kazi zao ndani ya mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Katika vipindi vichache vya kwanza, watazamaji walitambulishwa kwa wahusika, ambao ni pamoja na waigizaji kama Susan Kaittany ambaye ni mwanasheria wa zamani aliyegeuka kuwa mjasiriamali, na ambaye anamiliki duka la nywele na duka la kifahari la manukato. Vera Sidika ni mwanasosholaiti, mjasiriamali, na mwimbaji anayejulikana kwa biashara zake za Spa na chai ya Mitishamba.

Sonal Maherali ni mshawishi mashuhuri na mjasiriamali wa mitindo, ambaye pia ni mtetezi wa afya ya akili. Minnie Kariuki ni muigizaji, mjasiriamali, na staa wa filamu za uhalisia ambaye ameolewa na ana watoto wawili wa kike. Lisa Christoffersen ni mbunifu wa mapambo ya nyumba, mwandishi, dereva wa magari ya mbio, na mwanzilishi wa timu ya kwanza ya mbio za magari za wanawake pekee nchini Kenya.

Katika msururu mzima wa vipindi, watazamaji wameonyeshwa maisha ya kifahari ya wanawake hawa, wanapohudhuria karamu za kupendeza, na kuzozana juu ya tofauti za hadhi na haiba. Kutoka kwa mvutano ya Susan Kaittany na Minne Kariuki kwa Vera Sidika katika mzozo mkali wa kijinsia na Dkt. Maria kuhusu kutafuta kiki, kipindi hicho kimewafanya watazamaji kushikamana na Showmax kwa mchanganyiko wake wa drama, makabiliano, vichekesho na matukio ya kusisimua.

The Real Housewives of Nairobi imetayarishwa na Eugene Mbugua's D&R Studios (Young Rich Television) na ni sehemu ya kampuni ya The Real Housewives iliyopewa leseni kama umbizo na NBC Universal Formats, ambayo ni sehemu ya Universal International Studios, kitengo cha Universal Studio Group.

Ukiwa na Showmax, unaweza kutazama chochote unachotaka, wakati wowote, mahali popote kwenye Programu ya Showmax au tovuti ya Showmax. Ili kutazama sinema hii na mengine mengi tembelea Showmax.com leo ili kujiandikisha kuanzia kwa vifurushi vya chini vya hadi Kshs. 299.

Ili kupakua Showmax kwenye simu yako, nenda kwenye app store/play store kwenye kifaa chako, tafuta ‘Showmax’, chagua na upakue. Mara tu unapojiandikisha, utapewa chaguo zote za Showmax na Showmax Pro. Utapata ufikiaji wa papo hapo kwa burudani bora ya ndani na kimataifa.

Hakuna ratiba za TV. Hakuna mikataba. Hakuna majukumu. Hakuna matangazo. Hakuna ada za ziada za usakinishaji. Ukiwa na mpango wa kawaida wa Showmax au Showmax Pro, unaweza kutazama ukitumia vifaa kadhaa, ikijumuisha simu, kompyuta kibao (tablet), kompyuta, runinga  na media boxes..

Ukichagua mpango wa bei nafuu zaidi wa Showmax Mobile, unaweza kutazama kwenye kifaa chako cha mkononi au kompyuta kibao. Bila shaka, unaweza kuchagua kubadilisha mpango wako wakati wowote. Chaguo ni lako kabisa.