Bunge laidhinisha uteuzi wa Noordin Haji kama bosi wa NIS

Haji atakula kiapo chake siku zijazo akichukua nafasi ya Philip Kameru ambaye anatazamiwa kustaafu

Muhtasari
  • Kufuatia idhini ya Bunge, Haji sasa atarejea NIS ambako aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Kukabiliana na Uhalifu uliopangwa.
Noordin Haji akataa kutaja thamani ya utajiri wake
Noordin Haji akataa kutaja thamani ya utajiri wake
Image: Maktaba

Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mahusiano ya Kigeni imeidhinisha uteuzi wa Noordin Haji kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS).

Haji atakula kiapo chake siku zijazo akichukua nafasi ya Philip Kameru ambaye anatazamiwa kustaafu baada ya kushikilia afisi ya NIS tangu Septemba 2014.

Rais William Ruto, Mei 16, alimteua Haji kushika wadhifa wa NIS.

"Mheshimiwa Rais amewasilisha uteuzi huo kwa Bunge ili kuzingatiwa na Bunge, katika kutimiza matakwa ya kisheria yaliyowekwa chini ya Katiba na Sheria ya Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi," Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei alisema katika taarifa yake.

Kufuatia idhini ya Bunge, Haji sasa atarejea NIS ambako aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha Kukabiliana na Uhalifu uliopangwa.