Al Shabaab 20 wauawa Mandera, silaha zapatikana-Polisi

Maafisa hao walipelekwa katika hospitali ya eneo hilo kabla ya mpango wa kuhamishwa hadi Nairobi.

Muhtasari
  • Bunduki ndogo na RPG ni miongoni mwa vitu vilivyopatikana kwenye eneo la tukio.
Al Shabaab 20 wauawa katika mapigano Mandera, silaha zapatikana
Image: NPS/TWITTER

Takriban wanamgambo 20 wa al Shabaab waliuawa Jumatano jioni katika mapigano na kikosi maalum huko Mandera, polisi wamesema.

Msemaji wa polisi Dkt Resla Onyango alisema magaidi hao walivamia Kikosi cha Operesheni Maalum (SOG) katika eneo la Ogorwen kaunti ya Mandera na kusababisha mapigano.

"Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa majibizano makali ya risasi kati ya Maafisa waliokuwa doria na wanamgambo hao yalisababisha wanamgambo ishirini kujeruhiwa vibaya na Maafisa wanane wa NPS kujeruhiwa. Polisi pia walipata silaha za aina mbalimbali kutoka eneo la uhalifu,” Dk Resla alisema.

Maafisa hao walikuwa wakifuatilia genge hilo waliposhambuliwa kwa Rocket Propelled Grenade na kusababisha mapigano hayo.

Maafisa hao walipelekwa katika hospitali ya eneo hilo kabla ya mpango wa kuhamishwa hadi Nairobi.

Bunduki ndogo na RPG ni miongoni mwa vitu vilivyopatikana kwenye eneo la tukio.

Miili ya magaidi hao ilifanyiwa mazishi.

Vyombo vya usalama vya Kenya vimeongeza vita vyao dhidi ya wanamgambo wa al Shabaab wanaoendesha shughuli zao karibu na mpaka mkuu.