Wakazi wa Nairobi kujiandaa kwa wakati mgumu, ada zikiwemo za maegesho kuongezeka

Wakazi wa Nairobi watapata wakati mgumu ikiwa mswada utapitishwa

Muhtasari

•Maeneo ya maegesho magari na maduka kutarajia kupadishwa kwa kodi

Gavana Johnson Sakaja.
Gavana Johnson Sakaja.
Image: TWITTER

Wakazi wa kaunti ya Nairobi watalazimika kujiandaa kwa wakati mgumu huku serikali ya gavana Johnson Sakaja ikipanga kuongeza ada mbali mbali zikiwemo za maegesho ya magari. 

  Raia wa Nairobi watatarajiwa kuchimba zaidi mifukoni mwao ili kuwasilisha ushuru kwa serikali ya kaunti ikiwa mswada uliopendekezwa wa mapato utapitishwa.

Ikiwa imeainishwa katika Mswada wa Fedha wa Kaunti ya Jiji la Nairobi 2023, serikali ya kaunti inalenga kuongeza ada, tozo na adhabu kwenye mfumo wa usafiri wa jiji ikiwa ni pamoja na maeneo ya kuegesha magari, vituo vya  magari ya uchukuzi. 

Kaunti hiyo pia zaidi inalenga kuongeza ada za kukodisha maduka ya soko, mikahawa na maduka na maeneo ya umma. 

 Maeneo ya kuegesha magari yamegawanywa mara mbili eneo la kwanza likijumuisha katikati mwa jiji (CBD), Kijabe Street, Westlands, Upperhill, Community, Ngara, Highridge, Industrial area, Gigiri, Kilimani, Yaya Centre, Milimani, Hurligham, Lavington, Karen, Eastleigh, Muthaiga, Gikomba na Nairobi West. Maeneo ya pande II ni pamoja na maegesho ya barabarani katika vituo vya biashara, na maegesho yoyote ya soko la kaunti ambayo hayajajumuishwa katika pande ya I.

Katika maeneo ya pande I ada ya kila siku ya kuegesha magari ya gari dogo itaongezeka kutoka Ksh.200 hadi Ksh.300, magari ya kubebea mizigo ada itapanda kutoka Ksh.200 hadi Ksh.500, lori/basi dogo lenye uzito wa hadi tani 5 kupanda kutoka Ksh.1,000 hadi Ksh. Ksh.2,000, na kwa lori zaidi ya tani 5 kupanda kutoka Ksh.1,000 hadi Ksh.3,000.