Mtoto wa miaka 8 auawa na aliyekuwa mpenzi wa mamake

Mamake pia alikuwa ndani ya nyumba hiyo lakini alifanikiwa kutoroka na kurekodi taarifa kwa polisi.

Muhtasari

• Mshukiwa alifanikiwa kuingia ndani ya nyumba ya ya aliyekuwa mpenziwe ambapo alimuua mvulana huyo na kujaribu kumuua mfanyikazi wa nyumbani.

Crime scene
Crime scene
Image: HISANI

Jamaa mmoja amekamatwa na maafisa wa polisi katika kaunti ya Kiambu kwa madai ya kumuua mtoto wa miaka 8 wa aliyekuwa mpenziwake katika eneo la Ndenderu.

Kulingana na polisi, mshukiwa alifanikiwa kuingia ndani ya nyumba ya ya aliyekuwa mpenziwe ambapo alimuua mvulana huyo na kujaribu kumuua mfanyikazi wa nyumbani ambaye alitoa kamza kuwaita majirani.

Mshukiwa alipojaribu kutoroka, alianguka ndani ya shimo. Ilichukuwa juhudi za polisi na maafisa wa idara ya zima moto wa Kiambu kumuondoa mshukiwa shimoni.

Mamake mtoto aliyeuawa na ambaye alisemekana kuwa mpenzi wa kitambo wa mshukiwa pia alikuwa ndani ya nyumba hiyo lakini alifanikiwa kutoroka na kurekodi taarifa kwa polisi.

Yaya ambaye alijeruhiwa wakati wa shambulizi hilo alikimbizwa hospitalini na anapokea matibabu katika hospitali ya Kiambu Level 5 .