Kizaazaa Naivasha baada ya wanaume wawili kuanza kushikina kimapenzi hadharani

Shahidi mmoja alisema mambo yaliharibika wakati mmoja wa wanaume hao alipoamua kumfungua zipu mwenzake hadharani.

Muhtasari

•Mwaura alisema wananchi bado yameshangazwa na walichoona kwa sababu mmoja wa wanaume hao ameoa na ana familia.

Image: Getty Images

Kulikuwa na kizaazaa mjini Naivasha baada ya wakaazi kuwanasa wanaume wawili wakijivinjari katika baa moja huku wakishikana kimapenzi.

Wananchi hao waliokuwa na hasira waliwashambulia vibaya na kumjeruhi mmoja wao kabla ya wasamaria wema kuwaokoa.

Shida ilianza baada ya wawili hao waliokuwa wakifurahia kinywaji chao katika baa hiyo Jumanne jioni kuanza ‘kushikana visivyo’ hatua iliyowakera wateja wengine waliotazama kwa mshangao huku  ‘mapenzi’ hayo yakiendelea kunoga.

Kulingana na shahidi Paul Mwaura, kisa hicho kiliwaacha waliokuwa wakinywa pombe katika baa hiyo wakiwa na hasira huku wapenzi hao wawili wakiendelea na shughuli zao.

Mwaura aliongeza kuwa mambo yaliharibika wakati mmoja wa wanaume hao alipoamua kumfungua zipu mwenzake jambo lililowalazimu wateja wengine kuingilia kati.

"Wawili hao walikuwa wamelewa na kuamua kutaka kuanza maombo yao ya unyumba hadharani na kukasirisha wateja waliowafurusha nje  kabla ya kuwapiga vibaya," alisema.

Aliongeza kuwa katika miezi michache iliyopita, idadi ya wapenzi wa jinsia moja LBGTQ katika mji huo imeongezeka sana na wale wanaohusika kutumia nyumba za Airbnb.

Mwaura alisema wananchi bado yameshangazwa na walichoona kwa sababu mmoja wa wanaume hao ameoa na ana familia.

Afisa wa polisi ambaye alikataa kutajwa alisema kuwa kisa hicho hakijaripotiwa katika kituo cha polisi cha Naivasha.