Serikali yataka siku 30 zaidi kwa mazungumzo na madaktari

Madaktari wamegoma kwa zaidi ya siku 30 wakitaka serikali kutekeleza mkatabo wao.

Muhtasari

• Oduol alisema kumekuwa na changamoto kiasi kwani Baraza la Magavana bado halijawasilisha takwimu zinazohitajika kuhusu huduma za kiusalama za kiwango cha chini zaidi. 

Madaktari mjini Kisumu wakati wa maandamano Februari katika kuonyesha mshikamano na maafisa wa KMPDU waliofungwa jela wakati wa mgomo wa madaktari. Picha: FILE
Madaktari mjini Kisumu wakati wa maandamano Februari katika kuonyesha mshikamano na maafisa wa KMPDU waliofungwa jela wakati wa mgomo wa madaktari. Picha: FILE

Wagonjwa wanaotegemea huduma za afya katika hospitali za umma watalazimika kusubiri kwa muda zaidi baada ya Mwanasheria Mkuu kusema wanahitaji siku 30 zaidi kutatua mkwamo uliopo na madaktari wanaogoma. 

Akiwa mbele ya Hakimu Byrum Ongaya, Wakili Ochieng Oduol kutoka ofisi ya Mwanasheria mkuu alisema wamepiga hatua. 

Oduol hata hivyo alisema kumekuwa na changamoto kiasi kwani Baraza la Magavana bado halijawasilisha takwimu zinazohitajika kuhusu huduma za kiusalama za kiwango cha chini zaidi. 

Alisema ripoti ya taifa zima na maridhiano imependekeza pande zote zikiwemo CoG, hospitali za rufaa, muungano na wadau wengine kuendelea na mazungumzo ambayo ni maalum kwa kila kaunti. 

"AG anatambua uwiano mzuri unaohitajika hasa katika utoaji wa huduma za matibabu. Tunaomba uipe muda wa mahakama kuendelea kuwasiliana kwani utatuzi wa masuala yaliyopo ni muhimu na ya msingi," alisema. 

"Tunaomba siku 30 zaidi ili kukamilisha zoezi hili. Ni suluhu pekee ambalo limejadiliwa kwa nia njema litakalo toa suluhu la kudumu kwa mazingira ya viwanda yenye amani katika sekta hii," aliongeza. 

Suala hilo bado linaendelea huku wahusika wengine wakitoa mawasilisho yao kuhusu mchakato wa maridhiano.