Robert Burale awashauri wanandoa wachanga waliogundua ni ndugu

Burale alibainisha kuwa wawili hao walikuwa wachanga sana kuwa kwenye uhusiano na akasema kuwa hakubaliani na uhusiano huo.

Muhtasari
  • Wakati wa mahojiano na Oga Obinna, wenzi hao walibaini kuwa wanapendana sana na hawataachana.
Rober Burale na wapenzi; Brianna na Kyle
Image: Instagram

Mzungumzaji wa motisha Robert Burale amewashauri wanandoa hao wachanga, Kyle na Brianna, ambao waligundua kuwa walikuwa ndugu.

Wakati wa mahojiano na Oga Obinna, wenzi hao walibaini kuwa wanapendana sana na hawataachana.

Wapenzi  hao walibaini kuwa walipanga kuoana na kupata watoto.

Obinna alimwalika  Robert Burale ili kuwashauri jinsi ya kushughulikia suala lao.

"Ninataka waamue kuwa haya ndiyo mahojiano ya mwisho watakayowahi kufanya. Hawahitaji umaarufu kwa sasa, wanahitaji usaidizi, ushauri na maombi kwa sababu wao ni watu wema. Ngoja niwaambie kitu, hawataoana".

Baba wa mtoto mmoja alisema kwamba wenzi hao, Kyle na Brianna, walihitaji kuwasiliana na wazazi wao ili macho yao yafunguke.

“Wanatakiwa warudi pale mambo yalipoharibika, bwana aende akazungumze na Mungu pamoja na baba yake, kuna uchungu mwingi kwa huyu kijana, pia wanatakiwa kuzungumza na mama zao, kuna uchungu mkubwa. tatizo ikiwa mama zao wanajua kuwa wanachumbiana na wako sawa".

Burale alibainisha kuwa wawili hao walikuwa wachanga sana kuwa kwenye uhusiano na akasema kuwa hakubaliani na uhusiano huo.

"Kama hadithi hii ni ya kweli, kuna tatizo na kama si kweli basi bado kuna tatizo, kama ni kweli sikubaliani nayo. Miaka 21 na 19 ni mdogo sana. Wako kwenye umri ambao wanaishi maisha hawajui wanataka nini."

Burale aliendelea kusema; "Msichana anakomaa akiwa na miaka 24. mvulana akiwa na miaka 21, anajaribu kujitambua. Lakini kwa umri huo, hatakiwi kujitokeza kuongelelea baba yako vibaya. Sijui baba yake alimfanya nini, lakini ushahidi unasema hakuwepo, lakini watoto pia wanapaswa kuelewa kilichotokea kati yao na mama yao".

Burale alijitolea kuzungumza na kuwaombea nje ya kamera na pia alitaka kukutana na wazazi wa wanandoa hao.