Hali ya switofahamu katika uwanja wa ndege wa Dubai huku UAE na Oman zikikabiliwa na dhoruba mbaya

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai unasema unakabiliwa na "hali ngumu sana".

Muhtasari

• Katika maeneo ya kaskazini ya mbali, mwanamume mmoja alikufa gari lake liliposombwa na maji ya mafuriko.

Image: BBC

Mvua kubwa imenyesha katika mataifa ya Ghuba, na kusababisha mafuriko mabaya na pia kutatiza safari za ndege katika uwanja wa ndege wa pili kwa shughuli nyingi zaidi duniani.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai unasema unakabiliwa na "hali ngumu sana".

Mamlaka Iliwashauri baadhi ya abiria kutofika uwanjani hapo kwa kuwa maeneo mengi yamezingirwa na maji.

Katika maeneo ya kaskazini ya mbali, mwanamume mmoja alikufa gari lake liliposombwa na maji ya mafuriko.

Huko Oman, waokoaji walipata mwili wa msichana katika eneo la Saham, na kufanya idadi ya vifo nchini humo kufikia 19 tangu Jumapili.

Siku ya Jumatano, jumla ya safari 290 za ndege kwenda na kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai - kitovu kikuu cha kuunganisha safari za ndege kuelekea mabara tofauti - ziliahirishwa, kulingana na data ya Flight Aware saa tano usiku majira ya Afrka Mashariki.

Safari zingine za ndege 440 zilizochelewa, data ilionyesha. Uwanja huo wa ndege, ambao mwaka jana ulihudumia zaidi ya abiria milioni 80, wa pili baada ya Atlanta nchini Marekani, ulionya kuwa itachukua "muda" hali kurejelea ya kawaida.

Katika taarifa yake ya hivi punde iliwashauri wasafiri kutofika uwanjani hapo bila uthibitisho kutoka kwa mashirika ya ndege na kuzuia safari za kwenda uwanja wa ndege.