Polisi wamkamata mwanamume anayedaiwa kuwapiga risasi waandamanaji Mombasa

Katika taarifa kwenye jukwaa la X, polisi walisema tukio hilo liliacha watu kadhaa wakiuguza majeraha mabaya.

Muhtasari
  • Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa saba na nusu adhuhuri  katika eneo la Ganjoni mjini Mombasa wakati mmiliki wa duka anadaiwa kuwafyatulia risasi umati waliokuwa wakiandamana nje ya duka lake.
Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: HISANI

Polisi wamemkamata mwanamume anayedaiwa kuwapiga risasi waandamanaji mjini Mombasa siku ya Jumanne.

Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa saba na nusu adhuhuri  katika eneo la Ganjoni mjini Mombasa wakati mmiliki wa duka anadaiwa kuwafyatulia risasi umati waliokuwa wakiandamana nje ya duka lake.

Inasemekana kuwa 'alikerwa' na waandamanaji walioleta biashara kukwama kando ya barabara ya Nyerere.

Katika taarifa kwenye jukwaa la X, polisi walisema tukio hilo liliacha watu kadhaa wakiuguza majeraha mabaya.

"Mshukiwa amekamatwa, kupokonywa silaha na kuwekwa kizuizini," DCI alisema.

Polisi walisema watu wawili waliopata majeraha wanapokea msaada wa matibabu.

"DCI inawashukuru wananchi waliochukua hatua haraka kusaidia waliojeruhiwa hospitalini, na wakati huo huo inawaomba watu wa Mombasa kuwa watulivu kuhusu kesi hii kwani hatua muhimu za kisheria zinachukuliwa."

Polisi waliwazuia waandamanaji kwenda katika Ikulu ya Mombasa ambayo iko kando ya Barabara ya Mama Ngina.

Malori na magari ya polisi yalifunga barabara huku baadhi ya maafisa wakishika doria kwa miguu.

Asubuhi, maonyesho yalikuwa ya amani huku waandamanaji walianza kutembea kutoka Barabara ya Digo hadi Jomo Kenyatta Avenue kuzunguka eneo la Saba Saba kabla ya kurejea mjini.