Mwanamume afariki baada ya kurusha roho na mpenziwe mdogo kwa saa moja Kayole

Msichana huyo alikuwa amemwalika mpenzi wake kutoka Meru.

Muhtasari

•Wapenzi hao walikuwa wakijivinjari katika nyumba ya mwanadada mtaani Kayole wakati kisa hicho kilipotokea.

•Mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa kwenye kiti cha sofa wakati polisi na wapelelezi wa uhalifu walipofika katika eneo la tukio

Image: MALAYALAMEMAGAZINE.COM

Polisi wanachunguza tukio ambapo mwanamume wa miaka 47 alikufa baada ya kushiriki kipindi kizuri kitandani na mpenzi wake mdogo kwa saa moja Jumapili asubuhi.

Wapenzi hao walikuwa wakijivinjari katika nyumba ya mwanadada mtaani Kayole wakati kisa hicho kilipotokea.

Kulingana na ripoti ya polisi wa Kayole, msichana huyo alikuwa amemwalika mpenzi wake, Douglas Fundi Muthuri (marehemu) kutoka Meru.

"Walipokula chakula cha jioni walifanya urafiki wa karibu kwa saa moja na wakati wa tendo hilo, marehemu alipata shida ya kupumua kabla ya kuzimia," ilisema ripoti iliyoandikishwa katika Kaunti Ndogo ya Njiru.

Mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa kwenye kiti cha sofa wakati maafisa wa polisi na wapelelezi wa uhalifu walipofika katika eneo la tukio.

Polisi walipopekua mifuko ya suruali ya marehemu, walipata bahasha ndogo ya khaki iliyokuwa na pakiti ya furosemide na kidonge cha dawa ya bluu (viagra).

"Hakuna majeraha yanayoonekana kwenye mwili," inasoma ripoti hiyo.

Wapelelezi wa uhalifu kutoka Kayole walishughulikia eneo la tukio na kurekodi matukio kabla ya mwili wa marehemu kuhamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha jiji ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Mwanaume afariki baada ya kipindi cha saa moja kitandani na mpenziwe mdogo