Polisi wamsaka Didmus Barasa kwa madai ya kumuua dereva wa mpinzani wake

Barasa alimlenga msaidizi wa Khaemba, Brian Olunga na kumpiga risasi ya paji la uso

Muhtasari

•Barasa alikamatwa Jumanne jioni baada ya kuhusishwa na tukio la risasi ambalo lilisababishaa kifo cha msaidizi wa mpinzani wake.

• Barasa alichomoa bastola na kumlenga msaidizi wa Khaemba Brian Olunga na kumpiga risasi ya paji la uso

Image: FACEBOOK// DIDMUS BARASA

Polisi katika kaunti ya Bungoma wanamzuilia mbunge wa Kimilili Didmus Barasa kwa madai ya mauaji.

Barasa alikamatwa Jumanne jioni baada ya kuhusishwa na tukio la risasi ambalo lilisababishaa kifo cha msaidizi wa mpinzani wake.

Kisa hicho kilimhusisha Barasa na mpinzani wake Brian Khaemba wa DAP katika kituo cha kupigia kura cha Chebukwabi ambapo walipaswa kushuhudia shughuli ya kuhesabiwa kwa kura.

Mkuu wa DCI wa Bungoma Joseph Ondoro alisema kulitokea ugomvi kati ya wawili hao na kumfanya Khaemba kuondoka na kuelekea kwenye gari lake.

"Barasa alimfuata akiwa na wanaume wanne na kuwaamuru wasimruhusu (Khaemba) kuondoka mahali hapo lakini dereva wa Khaemba Joshua Nasokho alikaidi amri hiyo na kuwasha gari," alisema Ondoro.

Hapo ndipo Barasa alipochomoa bastola na kumlenga msaidizi wa Khaemba Brian Olunga na kumpiga risasi ya paji la uso.Olunga alifariki katika hospitali ya Kimilili Subcounty alipokuwa anapokea matibabu ya dharura.

Ondoro alisema wanamtafuta Barasa kwa ajili ya kuhoji kuhusu tukio hilo.

“Amekimbia lakini tunamtafuta. Ajisalimishe,” alisema.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika mochari ya hospitali ya Kimilili.