Sitaki handshake! Raila amzima Ruto na washirika wa Kenya Kwanza

Akizungumza Jumatatu, Raila alisema rais alitoa matamshi hayo wikendi.

Muhtasari
  • Ruto alisema hatakubali matakwa yake kwani Upinzani unafanya maandamano kuhusu ripoti ya wizi wa IEBC
KINARA WA AZIMIO RAILA ODINGA AKIWAHUTUBIA WAKEYA KATIKA UWANJA WA KAMUKUNJI 23/01/2023
Image: ANDREW KASUKU

Kiongozi wa Azimio-One Kenya, Raila Odinga amemjibu Rais William Ruto na washirika wake kuhusu madai ya kutaka handshake.

Akizungumza Jumatatu, Raila alikosoa matamshi hayo ambayo yalitolewa na upande wa Kenya Kwanza wikendi. 

Siku ya Jumapili, Ruto na washirika wake walidai kuwa mkutano wa Kamukunji ulikuwa mpango wa Raila kuchafua serikali ili kuafikiana naye.

Ruto alisema hatakubali matakwa yake kwani Upinzani unafanya maandamano kuhusu ripoti ya wizi wa IEBC.

“Sitaruhusu watu wachache kuwatendea Wakenya kwenye mikutano ili tuache kuwatumikia wananchi na kuwafanyia kazi. Mwisho umefika; hakuna zaidi. Ulichopata kutokana na vitisho kinafaa kutosha kwa sababu hatuwezi kufanya kazi kwa watu wachache mwaka hadi mwaka,” Rais alisema.

Raila alisema kwamba yuko tayari kukufa akipigania haki yake.

"Ruto na huyo Gachagua wake, wacheni upuzi , Kenya si yenu,Hatuwezi kutishwa na bwana Ruto na bwana Gachagua. Sisi ni wakenya na tutabaki Kenya hii. Wameiba ushindi wetu na sitaki waongeze matusi. Sisi tunadai haki yetu na tuko tayari kukufa kupigania haki yetu."Raila alisema.