Uchunguzi waanzishwa kuhusu ajali ya ndege ya watalii iliyoanguka Nakuru

Watatu ambao walikuwa ndani ya ndege walinusurika bila majeraha.

Muhtasari

•Ndege hiyo aina ya 5Y-C11 ilianguka Jumamosi jioni muda mfupi baada ya kuondoka uwanjani kuelekea Mara Kaskazini.

Image: NPS

Watu watatu walinusurika bila majeraha baada ya ndege ndogo kuanguka  katika eneo la Likia, kaunti ya Nakuru.

Ndege hiyo aina ya 5Y-C11 ilianguka Jumamosi jioni muda mfupi baada ya kuondoka uwanjani kuelekea Mara Kaskazini.

Polisi wameripoti kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani mmoja pamoja na abiria wawili wa kigeni wakati ilipohusika kwenye ajali.

"Wote watatu walitoroka bila majeraha. Uchunguzi wa vyombo husika kuhusu chanzo cha ajali hiyo umeanzishwa." Taarifa ya polisi ilisoma.

Abiria hao wanaripotiwa kuwa raia wa Peru na Ufaransa.