Wanadada wawili mahakamani kwa kuagiza vyakula vya 147,000 na kushindwa kulipa

Muhtasari

•Delilah Raila na Evy Cheptoo pia walishtakiwa kwa kusababisha drama kwenye Black Stars Lounge baada ya kuagizwa kulipa.

•Upande wa mashtaka ulisema wawili hao walitusi watu waliokuwa katika mkahawa huo kabla ya maafisa wa polisi kuitwa.

Delilah Raila na Evy Cheptoo katika mahakama ya Kibera mnamo Machi 14, 2022
Delilah Raila na Evy Cheptoo katika mahakama ya Kibera mnamo Machi 14, 2022
Image: CLAUSE MASIKA

Wanawake wawili walifikishwa katika mahakama ya Kibera siku ya Jumatatu baada ya kufurahia vyakula vya shilingi 147, 000 na kukosa kulipa bili.

Delilah Raila na Evy Cheptoo pia walishtakiwa kwa kusababisha drama kwenye Black Stars Lounge baada ya kuagizwa kulipa.

Vilevile wanadaiwa kutatiza amani pale  kwa kumtusi Gregory Nzamba na kundi la watu waliokuwa wakiburudika kwenye mkahawa huo mnamo Machi 6.

Wanaripotiwa kuagiza vyakula na vinywaji vya shilingi 147, 250 kisha wakakataa kulipa.

Upande wa mashtaka ulisema wawili hao walitusi watu waliokuwa katika mkahawa huo kabla ya maafisa wa polisi kuitwa.

Wasimamizi wa mkahawa huo ulilazimika kuomba usaidizi wa polisi kutoka kituo cha Kilimani baada ya kubaini kuwa wawili hao hawakuwa na nia ya kutoa pesa.

Raila na Cheptoo walikanusha mashtaka yote  mbele ya hakimuKibera Renee Kitagwa na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh30,000 kila mmoja.