Hali ilivyo, Mjengo wa mauti shule ya Precious Talent, NBI yatoa tamko

p1
p1

Wiki ya Tarehe 23 Septemba imeanza kwa wingu jeusi katika shule ya msingi ya Precious Talent.

Tukio hili la ajali limeripotiwa kuwaua wanafunzi 7 huku idadi kubwa kukumbwa na majeraha.

Wingu la simanzi limewagumbika walimu na wazazi wa shule ya msingi ya Precious Talent mtaani Dagoretti viunga vya jiji la Nairobi.

Soma hadithi nyingine;

Shule ya Precious Talent ipo katika wodi ya Ng'ando kaunti ya Nairobi.

Mtaa wa Ng'ando ni mtaa wa mabanda.

Ila je? Tukio hili lingeweza kuzuiwa ila lisitokee?

Mwanzo shule hii ina ukosefu wa miundo misingi ya kuwasetiri wanafunzi 800.

Mpangilio katika shule hii ni wa kufedhehesha mwanzo wanakosa ua la kuweka usalama.

Soma hadithi nyingine;

Taswira tunayoivuta katika vifusi ni bayana kuwa mjengo huu haukuwa dhabiti na imara.

Nguzo au miimili ya mbao iliyopinda ni ishara tosha kuwa jumba hili lingeporomoka.

Kuta zinazogawanya darasa sio mawe ila mbao nyepesi.

Mjengo kuu una ishara kuwa ulikuwa katika ujenzi bado.

Soma hadithi nyingine;

Mamlaka ya kitaifa inayohakiki mijengo inahoji kuwa jumba hilo ni "kazi iliyobuma na ukosefu wa ujuzi wa ujenzi"

Ni kweli kuwa mamlaka hii haina ufahamu wa mjengo kama huu katika rekodi zao.

Mashirika mbalimbali yameripotiwa kufika ili kusaidia katika juhudi za kuokoa maisha ya wanafunzi katika tukio hilo.

Wanafunzi 20 kwa sasa wametolewa katika vifusi vya mjengo huo na wapo katika hospitali kuu ya Kenyatta.