Hamisa kama unataka mimba ya Diamond tena Tuambie !timechoka na mehe mehe

NA NICKSON TOSI

Hamisa Mobetto amejitokeza na kutupilia mbali madai kuwa amerudiana na Diamond licha ya video katika mitandao kijamii kuenea zikionyesha wawili hao wakiwa katika malimwengu ya mahaba.

Hamisa aidha amejitete akisema kuwa wako na mtoto na Diamond swala ambalo linawafanya wawe pamoja kila wakati kama njia ya kupanga mikakati ya maisha ya baada ye.

Mobetto vile vile alisisitiza kuwa hana haja ya kuwa na Diamond tena na kuwa ameshajipanga kimaisha na mwanamume mwengine.

"Mimi na Diamond ni wapita njia tu,namheshimu kama baba wa mtoto wangu na huwa twazungumza kama mama na baba na hakuna kitu fiche wanachogawana''.alisema Hamisa

Aliongeza kuwa Diamiond ni mume anayependa wanawake na  hawezi taka tena kupoteza muda wake kwa mewanamume ambaye hana wakati na mwanamke mmoja kamwe.

"Diamond kiguuu na njia ,hatosheki na wanawake na mimi siwezi kutaka kupoteza muda wangu kwa mwanamume kama huyo ambaye hana haja na mwanamke mmoja ,nimemjua kwa muda sasa .aliongeza Hamisa

Tumekuwepo na gumzo katika mitandao kuwa wawili hao huenda wamerejeleana na kimahapa usemi ambao ameufutilia mbali Hamisa