Hamna mkutano wowote unaomkosoa Uhuru Kenyatta utakaofanyika mlima Kenya-Seneta Irungu Kang'ata atoa onyo

Seneta wa wengi wa Whip Irungu Kangata Jumanne alitoa onyo kwa viongozi ambao wameamua kuweka mikutano itakaompa changamoto rais Uhuru Kenyatta kama Kingpin katika mlima Kenya.

Kangata ambaye pia ni Seneta wa kaunti ya Murang'a alisema methali ya Kikuyu  inayosema kuwa mali ya mtu haiwezi rithiwa kama yuko hai.

"No meeting in any hotel or stadia can plot successfully to replace Our KINGPIN in Mt. Kenya. "Mundu ndagayagwo e muoyo!" Alisema Kangata.

Usemi wake unakuja baada ya kukutana na wanasiasa wa mlima kenya huku wakisema kuwa rais Uhuru Kenyatta ndiye kingpin na pia msemaji wa mlima Kenya.

Kangata alijiunga na kiongozi wa wengi katika bunge Amos Kimunya, gavana wa kaunti ya Meru Kiraitu Murungi miongoni mwa viongozi wengine katika mkutano huo.

Uongozi wa Kangata unaonekana kung'aa kwa miezi michache iliyopita hii ni baada ya kumuunga rais mkono baada ya wabunge wengi kuacha kumuunga mkono katika mlima kenya.