Handshake Mashakani –Huenda isidumu hadi 2022

bbi
bbi
Na Javas Bigambo

Mwafaka wa handshake kati ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani r Raila Odinga Huenda hautadumu hadi mwaka wa 2022 . makubaliano hayo yaonekana yalikuwa na malengo tofauti kwa viongozi hao wawili kwani kwa Raila ,lego lilikuwa kuhaisha azma yake ya kisiasa na kwa rais Kenyatta  dhamira ilikuwa kumthibiti Odinga kisiasa  ili kutuliza joto la kisiasa nchini na kuendelea na mipango yake ya maendeleo .

Matuko ya hivi karibuni yanafichua kwamba  mwafaka huo ulikuwa kuwahusu viongozi hao wawili kuendesha masuala yao ya kisiasa . wakati  kiranja wa walio wengi bungeni Irungu Kangata aliposema kwamba hawataunga mkono BBI endapo  hoja ya kupitisha mfumo wa ugavi wa mapato haingepitishwa ,alimaanisha kwamba hawakuwa ndani kwa miguu miwili katika mchakato mzima wa BBI .

Endapo upande wa serikali utagundua kwamba upinzani unasababisha msukosuko wa kila mara na haufuati mpangilio na matakwa yake basi huenda ukabadilisha nia na kuutupilia mbali mchakati mzima wa BBI .

Hatua ya wanasiasa kuwa tayari kuvutia upande wao na kutetea kabisa maslahi yao ni dhihirisho kwamba hawajali kabisa maslahi ya wakenya bali mchakato mzima wa BBI ulikuwa maigizo tu ya kusalia katika ulingo wa siasa .

Kufaulu kwa handshake sasa kutategemea jinsi kiongozi wa ODM Raila Odinga atakavyocheza karata zake za   kisiasa ili kuridhisha maslahi  ya kisiasa ya rais Kenyatta

Endapo hatafaulu kufanya hivyo basi Uhuru huenda asitake kuendelea na mchakato mzima wa BBI .BBI yaonekana ni mradi mzima wa Bwana Odinga kulingana na matamshi yake .

Pande zote mbili zitalazimika kutathmini  maslahi yazo kuhusiana na BBI .Uhuru sasa ndiye mwenye uwezo wa kujenga au kumaliza kabisa BBI .

Mtaalam huyu wa utawala alizungumza na gazeti la The Star